Mfanyabiashara: Usikose Hizi App Kwenye Simu Yako

Usikose Hizi App Kwenye Simu Yako

Hizi ni Apps ambazo zitakufanya uweze kukuza biashara na kukupatia wateja wengi zaidi.

Kwanza hakikisha una Apps za mitandao ya kijamii Whatsapp Business (Achana na ma_Gb whatsapp utakuja kulia) , Facebook, Instagram, Twitter (X) , Telegram Na Tiktok); Ukishakuwa nazo, hakikisha unakua Active sana.

Kisha kuwa na hizi App 5 Za Biashara.
.
1. Meta business suite.

Hii itakusaidia kuposti kipindi ambacho upo bize . Utaweza kuandaa posts za kupost wiki nzima au mwezi mzima ukaweka na muda kisha muda huo ukifika posts hizo zitajiposti kwenye akaunti yako zenyewe. Hii inasaidia unakua active kwenye kupostiwa pia inajibu Dm automatically za insta na Fb.

Pendekezo: Jinsi ya Kuandika Barua ya kuomba kazi (Mifano)

Hii App pia inakusaidia kufanya matangazo ya Sponsored Ads kwa usahihi na yanaruka Facebook na insta (kwenye YouTube Channel yangu nimekuwekea namna ya kuitumia na kufanya matangazo ya Sponsored ads yenye matokeo, Itafute youtube Link kwenye bio)
.
2. App ya Canva

Hii itakusaidia kudesign na kutengeneza poster zako za kila siku za kupost kwenye akaunti zako mitandaoni. Ukiweza kutumia app ya CANVA, utapunguza gharama nyingi sana za kulipa graphics designer mara kwa mara kukutengenezea matangazo, utatengeneza mwenyewe posts za kuvutia ( post zangu zote natumia hii App pia, Kwenye madarasa yangu whatsapp nafundisha kuitumia)
.
3. Thl accounting

Hii inakusaidia kutunza hesabu zako zote za biashara. itakusaidia kutengeneza invoice, itakusaidia kutunza hesabu za mauzo, mapato na matumizi.
Hata Kama uko mbali bado unaweza kuona mwenendo wa biashara yako. (Hizi App zipo nyingi hii ni mfano tu ni )
.
4. MPESA APP, TIGO APP Na AIRTEL MONEY APP au Halotel

Zitakusaidia kutengeza kadi za benki (Virtual mastercard) kupitia Mpesa yako au Airtel Money yako na kisha kufanya malipo ya Sponsored Ad. Ni vyepesi kuliko kutumia menu ya kawaida. Hizi App za fedha ni nzuri, pia zinatunza taarifa za miamala na wepesi wa kufanya malipo.
.
5. ENPASS password manager.

ENPASS password manager

Hii itakusaidia kutunza password zako za akaunti zako zote sehemu moja, inakusaidia kutunza kumbukumbu maana huwezi kukumbuka zote kwaio ni muhimu kuwa nayo katika simu yako.

Nasisitiza Tena kwa wewe mwenye Biashara usikose hizi app nzuri ya biashara.

Tunakutakia Biashara Njema !



Comments

Popular posts from this blog

Mrs Energy Ft Chino Kidd – Nimtaje