Wasifu wa DJ Feruuh, Nyimbo Zake Bora na Show Zake Kubwa
DJ Feruuh ni nani na ana miaka mingapi?
Jina la usani: DJ Feruuh
Jina halisi: Ally Mussa Maulid
Mix tapes zake ni za muziki gani: Taarab
DJ Feruuh alianzaje kazi yake ya kuwa DJ na lini?
DJ Feruuh alianza rasmi kazi yake ya kuDJ mwaka wa 2009 kule Zanzibar, Tanzania. Hivyo, anajivunia kuwa na tajriba ya zaidi ya miaka kumi na miwili katika kazi hii. DJ Feruuh anatambulika kwa kucheza kwenye vilabu tofauti tofauti Tanzania. Kwa sasa, ni mmoja wa madj tajika nchini Tanzania na eneo la Afrika Mashariki.
Kando na kucheza kwenye vilabu, DJ Feruuh pia amebarikiwa kufanya kazi na stesheni kadhaa za redio na televisheni . Kwenye miaka kumi na miwili aliokuwa kwenye kazi hii, DJ Feruuh amebahatika kufanya kazi na Breeze FM (Tanga), Coconut FM (Zanzibar) na Choice FM ( Dar es Salaam)
Mwaka wa 2015, alijiunga na Clouds FM na Clouds TV ambapo anafanya kazi hadi sasa.
Show zake kubwa ni kama gani?
- Leo Tena
- Trafik Jams
- Amplifaya na Millard Ayo
Amefanya Kazi wa Wasanii Wagani?
DJ Feruuh ndiye DJ rasmi wa mkurugenzi mkuu wa Kings Music Alikiba.
RELATED: Wasifu wa DJ YLB, Kazi Yake Kwenye Wasafi Media na Show Zake
Ngoma Zake Bora ni Kama Gani?
Kando na kucheza santuri, DJ Ferruh pia huachia nyimbo zake akiwashirikisha wasanii tajika kutoka Bongo. Nyimbo zake bora ni kama vile:
- Saula ft Mabantu
- Ukisimama ft B2K
- Sawa ft M.M.S
- Kinai ft Feisal
Show Zake Kubwa ni Kama Gani?
- Kila wiki DJ Feruuh hucheza santuri kwenye clouds TV siku ya Jumatatu hadi Ijumaa. Kwenye show hii, yeye hucheza muziki zote.
- Siku ya Ijumaa, DJ Feruuh ana kipindi kiitwacho ‘Wazee na Mbanga’ kwenye Clouds TV. Show hii inaanza saa tisa jioni hadi saa kumi na moja.
Comments
Post a Comment