App namba moja kwa huduma ya muziki barani Afrika, Boomplay imemtaja msanii Diamond Platnumz, kuwa ndio mwanamuziki aliyesikilizwa zaidi Tanzania, kulingana na taarifa rasmi za muziki mwaka 2019. Taarifa hiyo iliyowekwa kwenye ripoti maalumu kuhusu muziki imeegemea zaidi data kutoka kwenye app hiyo ya muziki ambayo ina watumia zaidi ya milioni 60, ulimwenguni kote huku Tanzania kukiwa na watumiaji zaidi ya milioni 4.2. Boomplay inajivunia kuwa na aina tofauti za nyimbo ambazo idadi yake ni zaidi ya milioni 20, ambazo zinapatikana kwenye iOS, Android na web. Nafasi ya pili imenyakuliwa na mwanadada Nandy, na ya tatu kuangukia kwake Harmonize huku Rayvanny akishika namba nne. Nae Aslay amekamata namba tano, huku namba sita ikinyakuliwa na Mbosso. Jux nae akainyakua nafasi ya saba huku Lava Lava akiijaza namba nane, mwanamuziki pekee wa injili katika orodha hii ni Joel Lwaga aliyeshika namba tisa na namba kumi akisimama mwanadada shupavu Vanessa Mdee. Mbali na wasanii, Boom...